1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIran

Iran yaalani Israel kukiri kuhusika na mauaji ya Haniyeh

25 Desemba 2024

Iran imelaani vikali hatua ya Israel kukiri kuhusika na mauaji ya aliyekuwa kiongozi wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran mapema mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4oYtv
Haniyeh | Sinwar | Gaza
Picha za viongozi wa Hamas waliouawa Ismail Haniyeh na Yahya Sinwar Picha: Marwan Naamani/dpa/picture alliance

Iran imekwenda mbali zaidi na kuituhumu Israel kwa kufanya kile walichokiita "uhalifu wa kinyama” na kutetea shambulio lake la makombora kama jibu.

Mnamo siku ya Jumatatu, Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz, alikiri kuwa nchi yake ilihusika na mauaji ya Haniyeh, ikiwa ni mara ya kwanza kwa afisa wa Israel kukiri rasmi.

Soma pia: Kifo cha Sinwar kinamaanisha ni kwa Hamas, Gaza, Lebanon?

Kabla ya hapo, Israel haikuwahi kukiri kuhusika na mauaji ya Haniyeh japo Iran na Hamas yenyewe iliihusisha Israel na kifo cha kiongozi huyo wa kisiasa wa Hamas.

Haniyeh, aliyekuwa anaongoza juhudi za mazungumzo ya kusitisha vita katika ukanda wa Gaza, aliuawa mjini Tehran mnamo Julai 31.