Iran yairuhusu IAEA kuongeza ukaguzi wa nyuklia
14 Desemba 2024Matangazo
Mkuu wa nishati ya nyuklia ya Iran, Mohammad Eslami amenukuliwa leo na shirika la habari la Iran, IRNA akisema kuwa wameongeza shughuli za nyuklia, hivyo kiwango cha ukaguzi kinapaswa kuongezeka. Matamshi ya Eslami yametolewa baada ya ripoti yaIAEA iliyoonekana na shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa, kusema kuwa Iran imekubali ombi la shirika hilo kuongeza kasi ya utekelezaji wa ukaguzi katika kiwanda cha kurutubisha madini ya urani cha Fordo, kilichoko kusini mwa Tehran. Wiki iliyopita, IAEA ilisema kuwa Iran imekifanyia marekebisho kiwanda cha Fordo, ili kiweze kuongeza kiwango cha uzalishaji wa urani iliyorutubishwa hadi asilimia 60, ambayo ni sawa na asilimia 90 inayohitajika kutengeneza silaha za nyuklia.