1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yawanyonga watatu kwa mauaji ya polisi

19 Mei 2023

Iran imewanyonga watu watatu waliokutwa na hatia ya kuwaua askari wa vikosi vya usalama wakati wa maandamano ya kupinga serikali yaliyofanyika mwezi Novemba mwaka jana.

https://p.dw.com/p/4RZLB
Iran hutumia kitanzi kutekeleza adhabu ya kifo
Iran hutumia kitanzi kutekeleza adhabu ya kifo Picha: Allison Bailey/NurPhoto/picture alliance

Hayo yameelezwa leo na tovuti rasmi ya mahakama ya Iran, Mizan.

Tovuti hiyo imewataja watu hao kuwa Majid Kazemi, Saleh Mirhashemi na Saeed Yaghoubi. Wote watatu walipatikana na hatia ya mauaji ya maafisa watatu wa usalama wa Iran mjini Isfahan.

Wakati wa mauaji hayo dola hilo la kiislamu lilikuwa linapambana na maandamano makubwa yaliyosababishwa na mauaji ya msichana wa Kikurdi Mahsa Amini mnamo Septemba 16.

Mahsa alikufa alipokuwa kizuizini baada ya kukamatwa kutokana na kile kilichoitwa kutojisitiri vizuri kama inayvotakiwa chini ya sheria ya taifa hilo.

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International, limesema watu hao waliteswa ili kukubali makosa hayo.