1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iraq yamuita balozi wake nyumbani kwa mashauriano

16 Januari 2024

Iraq imemuita balozi wake nyumbani kutoka Tehran kwa mashauriano baada ya jirani yake Iran kufanya mashambulizi kaskazini mwa Iraq yaliyosababisha vifo vya raia kadhaa.

https://p.dw.com/p/4bKLx
Irak Erbil | Trümmer nach Raketenangriff durch den Iran
Picha: AFP

Wizara ya mambo ya nje ya Iraq pia imemtaka balozi wa Iran mjini Baghdad kujieleza kufuatia mashambulizi hayo. 

Kupitia taarifa, wizara hiyo imesema kuwa, shambulio la Iran ni "ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya Iraq" na linakwenda kinyume na kanuni za ujirani mwema, sheria za kimataifa na pia kutishia usalama wa eneo hilo. 

Iraq yalaani mashambulizi ya Iran na kuyataja kama "mashambulizi dhidi ya mamlaka yake"

Iran ilirusha makombora jana Jumatatu na kulenga kile ilichosema ni makao makuu ya ujasusi wa Israel karibu na ubalozi mdogo wa Marekani katika mji mkuu wa jimbo la Kurdistan. Mashambulizi ya Iran pia yalilenga ngome za kundi linalojiita Dola la Kiislamu kaskazini mwa Syria.