SiasaSyria
Iraq yawarejesha makwao wakimbizi 625 kutoka kambi ya Syria
11 Machi 2024Matangazo
Msemaji wa Wizara ya Uhamiaji ya Iraq, Ali Abbas aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kwamba kambi ya Al-Hol inawahifadhi jamaa za watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Dola la Kiislamu pamoja na wakimbizi.
Amesema familia 157, au jumla ya watu 625 wamerejea Iraq kutoka Al-Hol siku ya Jumamosi katika juhudi za hivi karibuni za kuwarejesha makwao.
Zaidi ya Wasyria 43,000, Wairaq na wageni kutoka nchi zisizopungua 45 wanaishi katika kambi hiyo yenye hali ngumu na iliyojaa watu wengi kaskazini mashariki mwa Syria inayodhibitiwa na Wakurdi.