SiasaIsrael
UN yapitisha azimio la kufikishwa misaada ya kiutu Gaza
28 Oktoba 2023Matangazo
Mataifa 120 yameunga mkono azimio hilo lililoandaliwa na Jordan na kuungwa mkono na mataifa 22 ya Kiarabu. Mataifa 14 yalipinga azimio hilo ikiwa ni pamoja na Israel, Marekani na Australia. Mataifa 45 hayakupiga kura na Ujerumani, Italia na Uingereza yalijizuia.
Azimio hilo limetaka kufikiwa kwa makubaliano ya haraka ili kuruhusu misaada kuingia Gaza pamoja na kusitishwa kwa mapigano.
Israel imekosoa kwa ghadhabu pendekezo hilo, huku balozi wake kwenye Umoja wa Mataifa Gilad Erdan akiliita "takataka" na kusema Israel itaendelea kujilinda huku Hamas na Palestina wakilikaribisha.