SiasaIsrael
Israel imepitisha sheria itakayomlinda Netanyahu
23 Machi 2023Matangazo
Sheria hiyo imepitishwa huku waandamanaji wanaopinga mageuzi hayo wakiendeleza maandamano ya kupinga kile wanachokiona kuwa ni mwelekeo wa taifa kwenye utawala wa kimabavu.
Muungano wa Waziri mkuu Benjamin Netanyahu umeridhia sheria itakayomlinda kiongozi huyo wa Israel asionekane kuwa hafai kutawala kutokana na kesi yake ya rushwa na madai ya mgongano wa kimaslahi kuhusiana na ushiriki wake katika mabadiliko ya sheria.
Mabadiliko ya kisheria yamegawanya taifa kati ya wale wanaoiona sera mpya kama kuiondolea Israeli maadili yake ya kidemokrasia na wale ambao
wanadhani nchi imetawaliwa na uhura wa kimahakama.