1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel inasema Wapalestina 700,000 bado wapo kaskazini Gaza

Josephat Charo
17 Oktoba 2023

Jeshi la Israel limesema Wapalestina laki saba bado wako kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, huku likiendelea kuwatuma wanajeshi wake katika eneo la mpakani kabla operesheni ya ardhini kuanza.

https://p.dw.com/p/4Xcd1
Gazastreifen | Zerstörungen nach israelischen Vergeltungsluftangriffen
Mojawapo ya maeneo ya Ukanda wa Gaza kama anavyoonekana katika siku ya nane ya mashambulizi ya Israel kwenye ukanda huo.Picha: Middle East Images/ABACA/IMAGO

Msemaji wa jeshi la Israel, Jonathan Conrocus, amesema watu zaidi ya 600,000 wamehamia kusini mwa Gaza kufikia usiku wa Jumatatu (Oktoba 16) na bado mamia kwa maalfu ya wengine wanatakiwa waondoke kaskazini mwa Gaza.

Soma zaidi: Maelfu wakimbilia kusini mwa Gaza kukwepa jeshi la Israel

Afisi ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva imesema hatua ya Israel kuuzingira Ukanda wa Gaza na amri ya kuwataka Wapalestina waondoke huenda ikawa uhalifu wa kimataifa.

Soma zaidi: Rais Biden kuzuru Israel kwa mazungumzo na Netanyahu

Haya yanaripotiwa, wakati Rais Joe Biden wa Marekani akijiandaa kuitembelea Israel siku ya Jumatano (Oktoba 18).

Biden anatazamiwa kukutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Mfalme Abdullah wa Pili wa Jordan, Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Wapalestina na Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri katika juhudi za kuutuliza mzozo unaotishia kuliyumbisha eneo la Mashariki ya Kati.