Israel yaapa kujibu iwapo Iran itashambulia
12 Aprili 2024Watawala mjini Tehran wameitwika dhima Israel ya kuhusika na shambulizi hilo lililofanywa na ndege za kivita mnamo Aprili 1 kwenye ubalozi mjini Damascus na tangu wakati huo wameapa kwamba Iran italipa kwa kilichotokea. Kwenye shambulio hilo ambalo Marekani pia inaamini lilifanywa na Israel, makamanda wawili na makuruta wengine kadhaa wa jeshi la Iran waliuawa.
Israel katika hali ya tahadhari kufuatia kitisho cha Iran
Katika siku za karibuni Israel na Marekani zimekuwa kwenye hali ya juu ya tahadhari, zikiamini kwamba Iran inapanga kufanya mashambulizi kujibu kisa cha mjini Damascus.
Awali mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo mbili walizungumza kwa njia ya simu kujadili mashaka yaliyopo na kwa pamoja wamekubaliana kuvikabili vitisho kutoka dola hiyo ya Uajemi.