1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yadai kuwaua wanamgambo 300 wa Hamas Rafah

30 Mei 2024

Israel imesema vikosi vyake vimefanikiwa kuwaua wanamgambo 300 wa Kipalestina katika oparesheni yake ya kijeshi kwenye mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah iliyoanza mnamo Mei 6.

https://p.dw.com/p/4gT3g
Wapalestina wakiondoka katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza baada ya vikosi vya Israel kuendesha oparesheni ya kijeshi.ns
Wapalestina wakiondoka katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza baada ya vikosi vya Israel kuendesha oparesheni ya kijeshi.Picha: Abdel Kareem Hana/AP Photo/picture alliance

Takwimu hizo zimetolewa leo na msemaji wa serikali ya Israel, David Mencer huku wakaazi wa Rafah wakiarifu juu ya mashambulizi makali ya mabomu na mapambano ya bunduki, siku moja tangu Israel iliposema imechukua udhibiti wa njia muhimu inayoelekea katikati mwa mji huo. 

Wahudumu wa afya kwenye Ukanda wa Gaza wamesema mapambano yanayoendelea yamesababisha vifo vya watu 12 mapema leo Alfajiri ambao inaelezwa kwamba ni raia wa kawaida. 

Soma pia:Wahouthi kuendelea kuwaunga mkono Wapalestina

Israel imeendelea na kampeni yake ya kijeshi kwenye mji wa Rafah licha ya Mahakama ya Kimataifa ya utoaji haki ICJ kuimamuru nchi hiyo isitishe mashambulizi yake ambayo watawala mjini Tel Aviv wanasema yanalenga kuwaangamiza wapiganaji wa kundi la Hamas.