1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yafungua kivuko cha kuingiza misaada ya kiutu Gaza

12 Novemba 2024

Israel imetangaza kukifungua kivuko cha ziada cha kuingiza misaada ya kiutu katika Ukanda wa Gaza, kabla ya kufikia tarehe ya mwisho iliyowekwa na Marekani juu ya uboreshaji wa hali ya kibinadamu kwa Wapalestina.

https://p.dw.com/p/4mvgs
Mzozo wa Mashariki ya Kati
Israel yafungua kivuko cha kuingiza misaada ya kiutu GazaPicha: Jack Guez/AFP/Getty Images

Taarifa ya pamoja ya jeshi na idara inayohusika na masuala ya kiraia katika maeneo ya Wapalestina, imesema leo kuwa imekifungua kivuko cha Kissufim kama sehemu ya juhudi ya kuongeza kasi na njia ya kusambaza misaada katika Ukanda wa Gaza. 

Operesheni hiyo inajumuisha misaada ya vyakula, maji, vifaa vya matibabu na vile vya malazi ndani ya Gaza.

Mashambulizi ya Israel yauwa zaidi ya watu 20 Lebanon

Mwezi uliopita, mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa Marekani waliionya Israel kwamba, inao muda wa mwisho wa hadi kufikia Novemba 13, kuboresha hali ya usambazaji misaada ya kiutu, ama itakabiliwa na kuondolewa misaada ya kijeshi ya Marekani.