1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yakosoa Netanyahu kufananishwa na Hitler

26 Julai 2024

Israel imemkosoa mtaalamu wa Umoja wa Mataifa Francesca Albanese kwa kile ilichokitaja "chuki dhidi ya Wayahudi" baada ya kuweka chapisho mtandaoni akimfananisha waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Adolf Hitler.

https://p.dw.com/p/4in5I
Francesca Albanese
Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki katika ardhi za Palestina Francesca AlbanesePicha: Riccardo Antimiani/ANSA/picture alliance

Albanese alijibu chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X, lilionesha picha ya Hitler akisherehekewa na umati wa watu kwa salamu za Wanazi na vifijo juu ya picha ya Netanyahu aliyeonekana akilakiwa na wabunge wa Marekani wiki hii.

Katika chapisho hilo, Craig Mokhiber, afisa wa haki wa zamani wa Umoja wa Mataifa aliyejiuzulu Oktoba iliyopita aliandika 'historia inatazamwa kila wakati'

Vita vyaendelea Gaza, mchakato wa mazungumzo wakwama

Katika jibu lake, Albanese, mtaalamu huru aliyeteuliwa na Umoja huo wa Mataifa mwaka 2022 lakini asiyezungumza kwa niaba ya Umoja huo, alisema hicho ndicho alichokuwa akikifikiria siku hiyo.

Wizara ya ulinzi ya Israel ilijibu kwa haraka na kumkosoa huku ikisema haiwezekani kwamba Albanese bado anaruhusiwa kutumia Umoja wa Mataifa kama ngao kueneza chuki dhidi ya Wayahudi.