1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yathibitisha kumuua kamanda wa Fatah

21 Agosti 2024

Jeshi la Israel limethibitisha kumuua kamanda wa kundi la kijeshi la Fatah, Khalil al-Maqdah, likimtuhumu kwa kupanga mashambulizi katika Ukingo wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/4jkQs
Lebanon I shambulio la Israeli katika mji wa bandari wa kusini wa Sidoni
Mwanajeshi wa jeshi la Lebanon akipita mbele ya gari ambalo lilishambuliwa na Israeli katika mji wa bandari wa Sidon, Lebanon, Agosti 21, 2024.Picha: Mohammad Zaatari/AP/picture alliance

Taarifa ya jeshi hilo imeeleza kuwa al-Maqdah ameuawa leo katika shambulizi la anga katika eneo la Sidon, kusini mwa Lebanon. Israel imedai kuwa al-Maqdah ni kaka wa Mounir Maqdah anayeongoza kikosi cha mashahidi cha Al Aqsa, ambacho ni tawi la wapiganaji la chama cha Fatah, cha na imawatuhumu wote kwa kupanga mashambulizi na kufanya biashara ya magendo ya silaha kwenye eneo linalolikaliwa kimabavu na Israel la Ukingo wa Magharibi. Jeshi la Israellimesema ndugu hao walikuwa wakishirikiana kwa niaba ya Walinzi wa Mapinduzi wa Iran.