1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yawaamrisha watu kuhama katika maeneo zaidi ya Rafah

11 Mei 2024

Israel leo imetoa wito kwa Wapalestina katika maeneo zaidi ya mji wa Rafah kusini mwa Gaza kuhama na kuelekea kwenye kile inachokiita eneo la kibinadamu lililopanuliwa la Al-Mawasi

https://p.dw.com/p/4fjv3
Wapalestina waliopoteza makazi yao wawasili Khan Yunis baada ya kuondoka mjini Rafah, kusini mwa Gaza kutokana na agizo la Israel
Wapalestina waliopoteza makazi yao wawasili Khan Yunis baada ya kuondoka mjini Rafah, kusini mwa GazaPicha: picture alliance/dpa

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii X, msemaji wa jeshi la Israel ametoa wito kwa wakazi na watu waliopoteza makazi yao mjini Jabalia, eneo la kaskazini mwaGaza pamoja na na vitongoji vingine 11 katika ukanda huo, kuhamia mara moja kwenye makazi ya magharibi mwa mji wa Gaza City.

Wapalestina 24 wameuawa usiku wa kuamkia leo

Kulingana a shirika la habari la Palestina WAFA,  Wapalestina 24 waliuawa usiku wa kuamkia leo baada ya ndege za kivita za Israel kulenga maeneo kadhaa katikati mwa Gaza.

Israel yasema itaendelea na uvamizi wake mjini Rafah

Licha ya shinikizo kubwa la Marekani na wasiwasi ulioelezwa na wakazi na makundi ya kibinadamu, Israel imesema itaendelea na uvamizi wake mjini Rafah, ambapo zaidi ya watu milioni 1 wamekimbilia kutafuta hifadhi wakati wa vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas ambavyo vimedumu sasa kwa miezi saba.