Israel yazindua mpango wa mabadiliko ya sheria
14 Februari 2023Maelfu ya Waisrael wameandamana jana nje ya jengo la bunge dhidi ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu, wakati serikali yake ikizindua rasmi mpango tata wa kuufanyia mabadiliko mfumo wa kisheria wa nchi hiyo.
Maandamano hayo yafujo nje ya bunge la Israel Knesset, yakiambatana na kura ya vurugu ya kamati ndani ya jengo hilo, yalionekana kuongeza mgawiko kuhusu mpango wa Netanyahu.
Mpango huo umesababisha maandamano makubwa ya wiki kadhaa, kukoselewa na sehemu kubwa ya jamii ya Waisrael, na kutolewa taarifa ya wasiwasi kutoka kwa rais wa Marekani Joe Biden.
Soma pia:Maelfu waandamana Israel dhidi ya mageuzi ya Mahakama
Netanyahu na washirika wake wanasema majaji wa nchi hiyo wasiochaguliwa wana mamlaka makubwa zaidi na wanahitaji kudhibitiwa.
Wapinzani wake wanasema Netanyahu, ambaye anashtakiwa kwa rushwa, ana mgongano mkubwa wa maslahi.
Wanasema mpango wake wa mabadiliko utaharibu demokrasia ya nchi hiyo na usimamizi wa serikali, na kwamba ni njama yake ya kuondoa kesi yake ya uhalifu.