1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL: Maelfu ya watu watoa heshima zao za mwisho kwa mwandishi wa habari

23 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYT

Maelfu ya watu wakiwemo viongozi wa kidini wa Armenia na wanadiplomasia wa kigeni wamekusanyika mjini Istanbul kutoa heshima zao za mwisho kwa mwandishi wa habari raia wa Uturuki mwenye asili ya kiarmenia, Hrant Dink.

Dink aliuwawa kwa kupigwa risasi na kijana wa miaka 17 mwenye siasa kali za kizalendo.

Wakiwa wamevaa mavazi meusi waombolezaji walikusanyika nje ya ofisi za gazeti la Agos ambako Dink alipigwa risasi mara tatu Ijumaa mchana wiki iliyopita.

Dink atazikwa katika makaburi ya Waarmenia baada ya ibada nje ya ofisi ya gazeti alilolianzisha.