1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL:Mzozo wa kisiasa nchini Uturuki

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2M

Zaidi ya watu millioni moja waliandamana katika mji wa Izmir nchini Uturuki kuipinga serikali yao.

Maandamano hayo yaliitishwa na makundi yanayopinga utawala wa kidini kuishinikiza serikali ya chama chenye misingi ya kidini cha AK.

Wakosoaji wanasema chama tawala cha AK kina lengo la kuongeza ushawishi wa kidini katika jamii.

Maelfu ya polisi walipelekwa kwenye mji wa Izmir hapo jana kuzuia machafuko kwenye maandamano hayo yaliyofanyika siku moja baada ya shambulio la bomu lililofanywa kwenye soko moja na kusababisha kuuwa kwa mtu mmoja na 14 kujeruhiwa.

Maandamano ya jana yamefanyika baada ya maelfu ya watu kuandamana katika miji ya Ankara na Istanbul mwezi uliopita.Wandaaji wa maandamano hayo wanatumai matukio hayo yataviunganisha vyama vya upinzani kabla ya uchaguzi mkuu July 22.