1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL:Tayyip Erdogan awataka waturuki washikamane

1 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5i

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa mwito wa kuwepo umoja wa kitaifa katika suala tete la mzozo wa uchaguzi war ais mpya.

Akihutubia taifa kupitia televisheni Erdogan amesema nchi yake inaweza kukabiliana na matatizo yoyote ikiwa mshikamano utakuwepo.

Vyama vinavyounga mkono utengano wa dini na masuala ya siasawameitaka mahakama ya kikatiba nchini humo kutafakari ikiwa uchaguzi wa mgombea war ais bungeni wiki iliyopita ulikuwa wa halali.

Chama cha AK cha bwana Erdogan kilimtangaza waziri wa mambo ya nje Adullah Gul kuwa mgombea wake wa kiti cha urais mwishoni mwa juma mamia kwa maelfu ya waturuki walijitokeza kupinga uteuzi huo.