1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan: Gavana Koike ashinda muhula wa tatu madarakani

11 Julai 2024

Mwanamke wa kwanza kuongoza mji mkuu wa Japan Gavana wa Tokyo Yuriko Koike, ameshinda muhula wa tatu na kutetea nafasi yake madarakani akiendesha mojawapo ya miji yenye watu wengi zaidi ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4i6p9
Tokyo | Gavana Yuriko Koike
Gavana wa Tokyo Yuriko Koike, akiwa katika kampeni za kuwania tena.Picha: Hiro Komae/AP/picture alliance

Makumi ya wagombea walijitokeza kumvua wadhifa huo, miongoni mwao ni mbunge wa kike wa upinzani Renho Murata akiwa mmoja wa wapinzani wakuu, jambo ambalo ni nadra sana katika siasa za Japan zinazotawaliwa na wanaume. 

Katika wilaya 47 za nchini Japan, ni magavana wawili tu ambao ni wanawake. Katika ngazi ya kitaifa, uwiano unafanana, takriban 11% tu ya wajumbe katika bunge la taifa ni wanawake. Japan kwa sasa haina upendeleo wa jinsia kwa wanasiasa.

Kulingana na Mikiko Eto, profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Hosei, sheria kama hiyo itakuwa hatua muhimu zaidi katika kushughulikia usawa wa kijinsia.

Tofauti na Japan, mifumo mingi ya kisiasa duniani kote imetekeleza upendeleo wa kijinsia ili kuongeza idadi ya wanawake katika siasa.
Nchini Taiwan, ambako kuna viti vilivyotengwa kwa ajili ya wanawake na wagombea, wanawake sasa ni asilimia 41.6 ya bunge, ikiwa asilimia kubwa zaidi ya wabunge wanawake barani Asia.

Soma pia:Japan yafanikiwa kurusha roketi jipya katika anga ya mbali

Nchini Indonesia, uwakilishi wa wanawake bungeni ulikuwa mdogo sana kabla ya asilimia 30 ya mgawo wa kijinsia kuanzishwa. Mnamo 1999, chini ya mmoja kati ya wabunge 10 walikuwa wanawake. Miongo miwili baadaye, idadi hiyo imeongezeka hadi mmoja kati ya watano.

Nankyung Choi, msomi aliyebobea katika masuala ya wanawake na siasa Kusini-mashariki mwa Asia, aliiambia DW kwamba katika nchi ambazo uwakilishi wa kina wa wanawake bado uko chini sana, vitendo vya uthibitisho kama vile upendeleo wa kijinsia vinaonekana kuwa hatua ya kwanza kuchukua ili kubadili hali hiyo.

Usawa wa kijinsia katika utawala barani Asia

Mnamo mwaka wa 2023, India ilipitisha mswada wa kutenga 33% ya viti vya wanawake katika  bunge la kitaifa na vile vile katika mabunge ya serikali za mitaa.

Lakini mgawo huo haukutekelezwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Kwa hivyo kati ya wabunge 543 waliochaguliwa, ni 74 tu walikuwa wanawake ambayo ni takriban 14%.

Tokyo | Yuriko Koike
Gavana wa mji wa Tokyo Yuriko Koike,Picha: Yoshio Tsunoda/AFLO/IMAGO

Kwingineko katika bara hilo, viti 50 vimetengwa kwa ajili ya wanawake katika bunge la Bangladesh lenye wabunge 350.

Lakini ni takriban 5% tu ya wagombea waliojitokeza kuwania viti vingine katika uchaguzi wa mapema mwaka huu walikuwa wanawake, kulingana na takwimu zilizokusanywa na Muungano wa Mabunge.

Soma pia:Ndege ya abiria yashika moto ikitua uwanja wa ndege wa Tokyo

Kulingana na Choi,  Baadhi ya nchi barani Asia zimeweza kuongeza idadi ya wabunge wanawake wasio na upendeleo wa kijinsia, lakini haihusiani wazi na maendeleo ya kidemokrasia.

Choi ametolea mfano Singapore, karibu asilimia 30 ya wabunge ni wanawake, lakini takwimu hizo ni matokeo ya kile alichokiita "uamuzi wa serikali" inayoongozwa na People's Action Party kuteua wanawake zaidi bungeni ili kuongeza sifa zake dhaifu za demokrasia na shirikishi.

Ingawa upendeleo wa kijinsia unaweza kuwa umesababisha wanawake zaidi katika siasa, Choi anasema kuwa wasifu wa wale ambao wamefika kwenye nyadhifa za kufanya maamuzi pia unahitaji kujadiliwa.

Tafiti: Wabunge wengi Asia ni wanawake

Baadhi ya tafiti linganishi zinaonyesha kuwa wabunge wengi wanawake barani Asia ni wanawake wa makamo, wasomi na walio na weledi na kuwaacha nje wanawake vijana wanaoishi maisha ya wastani.

India | Bunge likiwa katika vikao vyake
Bungela India likiwa katika vikao vyakePicha: AP Photo/picture alliance

Hata hivyi Choi ameonya kwamba kuwa na wanawake wengi bungeni ni suala moja, na nis swala tofauti katika kutathmini kama hatua hiyo imetafsiri katika maendeleo yoyote ya maana katika usawa wa kijinsia.

Kulingana na Chang- Ling Huang, profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Taiwan,  Kwa upande wa Taiwan, hata kukiwa na zaidi ya asilimia 40 ya wabunge wanawake, juhudi za wabunge kuwakilisha maslahi ya wanawake ni muhimu lakini hazitoshi kwani mtazamo wa tawi kuu la serikali bado ni jambo la msingi.

Licha ya hatua za hivi karibu za idadi ya wanawake bungeni, uwepo wao katika nyadhifa za juu bado ni mdogo. Sehemu ya mawaziri wanawake katika Baraza la Mawaziri  Asia ya Kati na Kusini ni 9.5% - idadi ya chini kabisa, kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Wanawake iliyopewa jina  "Viongozi wa Kisiasa Wanawake 2024."

Soma pia:Mzozo wa Mashariki ya kati wagubika mkutano wa G7 Tokyo

Kwa sasa, Bangladesh ina wanawake wawili tu wanaoongoza wizara, mmoja wao ni waziri mkuu mwenyewe. Katika Baraza jipya la Mawaziri la Pakistan baada ya uchaguzi wa Februari, kuna mwanamke mmoja tu.

Choi anasema ukosefu wa uongozi wa kike unatokana na utamaduni wa mfumo dume uliopo na kukua kwa vuguvugu la kihafidhina katika kanda hiyo.