JangaJapan
Japan yatangaza tahadhari ya tsunami
1 Januari 2024Matangazo
Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Japan imesema tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.6 kwa kipimo cha Richter limeathiri zaidi miji ya Toyama, Ishikawa na Niigata, yote kwenye kisiwa chake kikubwa cha Honshu kilicho kwenye mwambao wa magharibi wa Bahari ya Japan.
Shirika la habari la Urusi, TASS, limewanukuu mameya wa miji ya Vladivostok na Nakhodka wakitangaza tahadhari ya tsunami katika maeneo hayo yaliyo kwenye kisiwa cha Sakhalin.
Soma pia: Istanbul yapigwa na tetemeko la ardhi
Onyo la mawimbi yenye ukubwa wa mita tatu lilitolewa pia kwenye baadhi ya maeneo ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.
Serikali mjini Seoul iliwataka wakaazi wa miji ya mwambao wa mashariki kuchukuwa tahadhari ya kupanda kwa viwango vya bahari.