Japan yawakumbuka wahanga wa Fukushima
11 Machi 2023TOKYO
Madhimisho hayo yamefanyika huku uungwaji mkono wa umma wa matumizi ya nishati ya nyuklia ukiongezeka na kumbukumbu ya mkasa huo wa 2011 zikififia. Kanda za televisheni zilionyesha watu waliopoteza wapendwa wao kwenye tsunami hiyo wakiweka maua na kusali mbele ya makaburi yao.
Tetemeko kubwa la chini ya bahari la ukumbwa wa 9.0 katika kipimo cha ritcha, la nne kwa ukubwa kurekodiwa katika historia ya dunia, liliharibu eneo la Kaskazini Mashariki mwa Japan miaka 12 iliyopita. Tetemeko hilo lilisababisha tsunami iliyosababisha vifo vya takriban watu 18,500 na wengine kupotea pamoja na kuzidiwa nguvu kwa mifumo ya kupoza kwenye kinu cha Fukushima Daiichi, na kusababisha maafa makubwa zaidi ya nyuklia tangu yaloyoshuhudiwa katika kinu cha Chernobyl.