Raila Odinga ni mwanasiasa mkongwe aliyeingia katika historia ya kuangushwa katika uchaguzi wa rais. Tangu mwaka 1997 ameshaangushwa mara tano, mara hii ameangushwa na William Samoei Ruto. Je umefika wakati wa mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 77 kuachana na siasa? Sikiliza mahojiano kati ya Saumu Mwasimba na mchambuzi wa kisiasa kutoka Nairobi Dr. Alutalala Mukwana.