Israel yashambulia kituo cha kuongoza vita cha Hamas
14 Desemba 2024Taarifa hiyo iliongeza kwa kusema wanamgambo walikuwa katika mipango ya kuishambulia Israel na kueleza kuwa kundi hilo lilikuwa limejibanza katika eneo ambalo awali lilifahamika kama "Shule ya Yaffa" mjini Gaza.Hata hivyo madai hayo hayakuweza kuthibitishwa mara moja. Mara kadhaa jeshi la Israel limekuwa likisema Hamas wanajificha katika miundombinu ya kiraia, kama shule, hospitali na kuwatumia Wapalestina kana ngao ya kivita, katika ukiukwaji wa sheria za kimataifa. Na kwa shambulizi hilila sasa hakutoa taarifa ya athari zake. Mzozo wa sasa ulianza baada ya Hamas na vikundi vingine kuvamiwa Israel Oktoba 7, 2023, kuua watu 1,200 na kuchukua mateka 250. Na Israel ilianzisha mashambulizi ya kulipiza kisasai kikubwa ambacho, mamlaka za Palestina wamesema, wameua zaidi ya 44,800 huko Gaza tangu wakati huo.