1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Jeshi la Sudan laonya kuhusiana na kuzuka kwa machafuko

13 Aprili 2023

Jeshi la Sudan limetahadharisha leo kuhusiana na machafuko yanayoweza kutokea kati yake na kikosi chenye nguvu cha wapiganaji wa kiraia walioungana kulisaidia jeshi RSF, ambacho wanasema kimetuma vikosi katika mji mkuu.

https://p.dw.com/p/4PzPf
Sudan | Proteste in gegen die Militärherrschaft Khartoum
Picha: Marwan Ali/AP/dpa/picture alliance

Katika taarifa, jeshi la Sudan limesema kupelekwa kwa vikosi vya RSF mjini Khartoum na kwengineko nchini humo, kumefanyika bila idhini au ushirikishwaji wa uongozi wa jeshi.

Jeshi hilo linasema hatua hiyo ya RSF imesababisha taharuki na hofu miongoni mwa watu na kuzidisha hatari ya usalama na kuongeza mivutano na jeshi la kawaida.

Mivutano kati ya jeshi la RSF imeongezeka katika miezi ya hivi majuzi, jambo lililosababisha kucheleweshwa kutiwa saini kwa mkataba unaoungwa mkono kimataifa wa kuirudisha nchi hiyo katika utawala wa kidemokrasia.