Syria ilitumia gesi za kemikali kushambulia wapinzani - OPCW
27 Januari 2023Matangazo
Watu 43 waliauwa katika shambullizi hilo.
Ripoti ya shirika hilo iliyotolewa leo, imethibitisha kuwa utawala wa Rais Bashar Al-Assad ulitumia silaha za kemikali wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
Mkurugenzi Mkuu wa OPCW, Fernando Arias, amesema matumizi ya silaha za kemikali Douma na kwengineko hayakubaliki na yanakiuka sheria za kimataifa.
Syria ambayo ilijiunga na OPCW mwaka 2013 kutokana na shinikizo la jumuia ya kimataifa baada ya kulaumiwa kwa shambulizi jengine la silaha za kemikali, haitambui mamlaka ya timu ya uchunguzi na mara kwa mara imekana kutumia silaha za kemikali.