Jeshi la Urusi ladai kuuteka mji mmoja mashariki mwa Ukraine
8 Septemba 2024Katika taarifa, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema kuwa vikosi vya nchi hiyo vimeuteka mji huo wa Novohrodivka katika eneo la Donetsk, umbali wa kilomita 20 kutoka mji wa Pokrovsk.
Mji huo ulikuwa na zaidi ya wakazi 14,000 kabla ya kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari mwaka 2022, hii ikiwa ni kulingana na takwimu rasmi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amteuwa mshauri wa nje wa masuala ya kimkakati
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, leo amemteuwa aliyekuwa waziri wa viwanda vya silaha, Oleksandr Kamyshin, kama mshauri wa nje wa masuala ya kimkakati. Haya ni kwa mujibu wa amri iliyochapishwa kwenye tovuti ya urais.
Kamyshin, alijiuzulu kama waziri wiki iliyopita kama sehemu ya mabadiliko kwenye serikali ya Ukraine katika wakati mgumu wa vita vyake na Urusi.