1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jimmy Carter asema kundi la Hamas liko tayari kuitambua Israel

Kalyango Siraj21 Aprili 2008

Lakini limetoa masharti kadhaa ambayo kwanza yatekelezwe

https://p.dw.com/p/Dlsl
Rais wa Syria Bashar Assad akutana na rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter mjini Damascus Ijumaa Friday, 18, 2008. Carter amekutana na kionmgozi wa Hamas alioko uhamishoni Damascus Khaled Mashaal.Picha: AP/DW

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter amesema kuwa kundi la kiislamu lenye msimamo mkali katika Palestina la Hamas linasema kuwa liko tayari kukubali mkataba wa amani kwa masharti kuwa ikiwa mkataba huo utaidhinishwa na wananchi wa Palestina kupitia kura.

Bw Carter ametoa kauli hiyo leo jumatatu mjini Jerusalem wakati akizungumza na waandishi habari.

Jimmy Carter ametoa kauli hiyo baada ya kukutana mara mbili na kiongozi wa hamas alioko uhamishoni Khaled Meshaal mjini Damscus Syria.

Mkutano wake huu na kiongozi huyo wa Hamas umezikasirisha Marekani pamoja na Israel ambazo zinalichukulia kundi hilo kama kundi la kigaidi japo lilishinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2006.

Akizungumza mjini Jerusalem mbele ya mkutano wa shirika la baraza la Israel linalohusiana na masuala ya nje,rais huyo wa zamani wa Marekani amesema kuwa,kundi la Hamas litakubali taifa la Palestina kufuatna na mipka ya mwaka wa 1967 na ikiwa limekubaliwa na watu wa Palestina.Aidha akaongeza kuwa ameambiwa na kundi hilo kuwa liko tayari kulikubalia taifa la Israel kuishi kama jirani mwema.

Haikubainishwa ikiwa Hamas litahitaji kura ya maoni kuwahusisha wakimbizi wa kipalestina wanaoishi nje ya ukanda wa Gaza pamoja na ukingo wa magharibi wa mto Jordan.

Yeye Bw Carter ameongeza kuwa kundi hilo pia litakubali makubaliano yoyote ambayo yamefikiwa na serikali ya mseto ikiundwa na kundi la Hamas na la Fatah la linaloongozwa na Mahmud Abbas.

Hata hivyo Bw Carter ametilia mkazo kuwa hakuna mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa na mazungumzo ya amani yanayosimamiwa na Marekani tangu yarejelelewe upya mwezi Novemba,huku waPalestina wakiendelea kukasirishwa na kuendelezwa kwa makazi ya kiyahudi katika ardhi inayokaliwa ya ukingo wa magharibi.

Matamshi yake pamoja na hatua yake ya kukutana na kiongozi wa Hamas yamekosolewa vikali na Israel.

Naibu waziri mkuu wa Israel,Shaul Mofaz,ameiambia Radio moja ya Israel kuwa Jimmy Carter hajui kinachoendelea,na anazunguzia tu upande mmoja.Anazungumza na Khaled Meshaal na kujaribu kupata mkataba huku mashambulizi ya kinyama yanaendelezwa dhidi ya taifa la Israel.

Kuhusu suala hilo mchambuzi mmoja wa hapa Ujerumani kutoka taasisi ya sayansi na siasa ya Ujerumani Dr Patric Muller,ameiambia DW kuwa yaonekana kundi la Hamas limebadilika kidogo.

Mkutano wa Carter na kundi la Hamas umepingwa vikali na Marekani pamoja na Israel yakisema kuwa ni makosa kufanya hivyo.Yeye Carter amesema kulitenga kundi hilo katika mchakato mzima wa kuleta amani ni makosa sana.

Ameongeza kuwa kundi hilo pia limekubali kumruhusu mwanajeshi mmoja wa Israel alietekwa Juni mwaka wa 2006,Gilad Shalit kuwaandikia barua wazazi wake.

Rais huyo wa zamani wa Marekani amekamilisha ziara yake ya siku tisa katika mashariki ya kati.Ametembelea nchi za Saudi Arabia,Syria,Jordan,Misri na ukingo wa magharibi wa mto Jordan.