Asili na mazingiraPapua New Guinea
Uokoaji wasitishwa eneo la maporomoko Papua New Guinea
5 Juni 2024Matangazo
Meja Joe Aku, mmoja wa maafisa wakuu wa kijeshi wanaosimamia eneo hilo la mkasa, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba juhudi zote za kupata miili hiyo zimesitishwa kwa sababu ya hatari hiyo na kuonya kutokea kwa maporomoko zaidi ya ardhi. Aku, ameongeza kuwa eneo hilo litafungwa kwa muda usiojulikana. Serikali ya Papua New Guineainakadiria watu 2,000 wanaweza kuwa wamezikwa katika maporomoko hayo ya urefu wa mita 600, lakini kulingana na Aku, idadi hiyo inaweza kuwa takribani 650 huku mamlaka ya afya katika eneo hilo ikisema juhudi za muda za uokoaji ziliwezesha kupatikana kwa miili tisa tu.