1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za upatanishi kati ya Israel na Hamas zinaendelea

5 Desemba 2023

Juhudi za upatanishi za kujaribu kufufua mpango wa kusitisha vita na kutowa nafasi ya ubadilishanaji mateka na wafungwa, kati ya Israel na Gaza zinaendelea.

https://p.dw.com/p/4ZobB
Nahostkonflikt | Nasser Klinik in Chan Junis
Picha: Ibraheem Abu Mustafa/REUTERS

Lengo kuu katika mchakato huo ni kufikiwa makubaliano ya kumaliza kabisa vita kwa mujibu wa waziri mkuu wa Qatar Mohammed bin AbdulRahmani al Thani. Mjumbe huyo ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Qatar amesema Misri na Marekani pia zinaendelea kushirikishwa katika mazungumzo. Mapigano kati ya Israel na Hamasyalianzatena Ijumaa wiki iliyopita baada ya kusitishwa kwa wiki moja. Vyombo vya habari vya Israel leo vilisema kwamba vikosi vya nchi hiyo vimeendelea kushambulia katika maeneo ya karibu na mji wa Khan Younis Kusini mwa Gaza.Kwa upande mwingine mfalme Abdullah wa Jordan amesema ulimwengu unapaswa kulaani jaribio lolote la Israel la kutaka kuweka mazingira yatakayowalazimisha Waoalestina kukosa makaazi ndani ya Ukanda wa Gaza au nje ya mipaka yao.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW