1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Jukumu la kihistoria la Ufaransa katika mzozo wa Haiti

Louis Lisa
25 Machi 2024

Ghasia za magenge ya wahalifu zimeongezeka katika nchi maskini ya Haiti, kwenye kanda ya Karibiani. Lakini mzozo huo unakwenda mbali zaidi tangu enzi za Haiti ilivyokuwa koloni la zamani la Ufaransa

https://p.dw.com/p/4e6b7
Haiti |Port-au-Prince
Hali ilivyo mjini Port-au-PrincePicha: Odelyn Joseph/AP/dpa/picture alliance

Umaskini, vurugu za kisiasa na uhalifu wa kiwango cha juu, vimelikabili taifa hilo la Caribbean kwa miongo kadhaa. Hivi sasa, ghasia zimeongezeka na kushindwa kudhibitiwa.

Mnamo Februari 29, kaimu waziri mkuu Ariel Henry alitangaza uchaguzi mpya utakaofanyika Agosti 2025. Muhula wake mamlakani ulipaswa kumalizika mwishoni mwa Februari, na hivyo tangazo lake lilitafsiriwa na magenge ya kihalifu, kama wito wa kushika silaha.

Ufaransa kuwaondoa raia wake Haiti kufuatia machafuko

Magenge hayo yalivamia ikulu ya kitaifa na magereza, na kusababisha wafungwa 3,000 kutoroka. Magenge hayo kwa kiasi kikubwa yanadhibiti maeneo makubwa ya mji mkuu wa Port-au-Prince na maelfu ya wakaazi wamekimbia. Ufaransa ambayo ni mtawala wa zamani wa taifa hilo inalo jukumu kubwa la kihistoria katika mzozo wa sasa.

Wanajeshi wa Jamhuri ya Dominican
Wanajeshi wa Jamhuri ya Dominican wakisimamia zoezi la raia wa Haiti wanaokimbia mapiganoPicha: Fran Afonso/REUTERS

Mapinduzi ya Haiti

Mnamo mwaka 1804, Haiti iliandika historia baada ya kuwa taifa la kwanza katika eneo la Amerika ya Kusini na Karibiani kupata uhuru, uliotokana na mapinduzi ya Haiti, yaliyowezeshwa na uasi uliofanywa na watumwa. Lakini baadae mwaka 1825, Ufaransa ilitangaza kwamba itatambua tu uhuru wa Haiti kwa gharama ya faranga milioni 150, sawa na takriban mara tatu ya Pato la Taifa la Haiti wakati huo. Ufaransa pia ilisema ushuru wa kuagiza bidhaa za Ufaransa ulipaswa kupunguzwa kwa nusu. Haiti ililazimika kukopa pesa kutoka benki za Ufaransa, kwa viwango vya juu vya riba ili kulipa deni. Wachumi wanalitaja kuwa  "deni mara mbili" na Haiti iliweza kulipa deni lake kufikia mwaka 1947.

Fuatilia: Kiongozi wa genge la wahalifu nchini Haiti Ti Greg auawa

Magenge ya wahalifu yawahangaisha raia Haiti

Mwanahistoria na mkuu wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa utumwa chenye makao yake makuu mjini Paris Ufaransa, Myriam Cottias, anasema nchi ambazo zilijikomboa kutoka katika utumwa zilijitahidi kujifikiria kuwa jamii zenye watu sawa. Aliieleza DW  kwamba "utumwa unajenga uwanja wa kukosekana kwa utulivu wa kisiasa, na migawanyiko katika jamii inayosababishwa na utumwa haipotei. Anaeleza kwamba hata leo, Haiti ina wasomi mafisadi na idadi ya watu ambayo kwa kiasi kikubwa imesalia kuwa maskini sana."

Mapinduzi ya Ufaransa

Jean Fritzner Etienne ambaye ni mwanahistoria wa Haiti katika Chuo Kikuu cha Paris 8, anasema madeni ya Haiti yalisaidia kuimarisha miundo ya mamlaka ya uongozi. "Wahaiti walitiwa moyo na mapinduzi ya Ufaransa, ambayo yalikuwa yamefanyika muda mfupi kabla ya miaka ya 1789. ... lakini Wafaransa hawakutumia kanuni za mapinduzi yao wenyewe za uhuru, usawa, udugu na haki za binadamu nje ya mipaka yao wenyewe."Haiti yaendelea kukabiliana na magenge ya uhalifu

Mwanahistoria huyo anasema Marekani, ambayo iliikalia kwa mabavu Haiti kuanzia 1915 hadi 1934, iliimarisha zaidi dhana kwamba nchi hiyo ni "duni." 

"Kuanzia mwaka 1957 hadi 1986, iliunga mkono udikteta katili wa Francois, na baadaye Jean-Claude, Duvalier, aliyejulikana kama 'Papa Doc' na 'Baby Doc. Na inaendelea kuingilia masuala ya ndani hadi leo."

Mazungumzo ya kuunda serikali yashika kasi nchini Haiti

Haiti Port-au-Prince
Watu wakiwa wamekusanyika karibu na eneo kulikofanyika uhalifuPicha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Mnamo Aprili 2003, Rais Jean-Bertrand Aristide alitaka serikali ya Ufaransa ilipe deni mara moja iliyokuwa imewekewa Haiti. Wakati huo, deni hilo lingekuwa karibu dola bilioni 22. Mwaka mmoja hivi baadaye, Aristide alipinduliwa katika mapinduzi yaliyoandaliwa na Ufaransa na Marekani. Ilipoulizwa na DW katika mkutano na waandishi wa habari hivi majuzi kama kulikuwa na dhamira yoyote ya kulipa deni hilo, wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilijibu kwamba suala hilo "halijajadiliwa kwa sasa."Hofu yatanda Haiti katikati ya mkwamo wa kisiasa

Wachambuzi wana hofu kama Ufaransa itaweza kurejesha fedha hizo. Laurent Giacobbi kutoka taasisi ya kimataifa ya masuala ya kimkakati ya Ufaransa IRIS, anasema hakuna mkoloni wa zamani anaweza kufanya hivyo.

Lakini mtaalamu mwingine anayeitwa Frederic Thomas kutoka kituo cha kujitegemea cha Tricontinental nchini Ubelgiji, anasema jumuiya ya kimataifa imechangia moja kwa moja katika hali ya sasa kwa kumuunga mkono Henry, ambaye hakuwa maarufu tangu mwanzo, baada yakuuawa kwa Rais Jovenel MoiseJulai 2021.