Jumuiya ya kimataifa yalaani mapinduzi Mali
20 Agosti 2020Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Marekani na baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zote zimetaka uongozi huo wa kijeshi kumwachia huru rais Ibrahim Boubacar Keita , waziri mkuu Boubou Cisse na wengine ambao wamekamatwa katika mapinduzi yaliyofanyika siku ya Jumanne kufuatia maandamano ya miezi kadhaa.
Katika mji mkuu wa Mali Bamako, Goita alisema baada ya kukutana na watendaji wakuu wa kiraia kuwa yeye ndio kiongozi wa "kamati ya taifa kwa ajili ya uokozi wa umma" ambayo imekamata madaraka.
"Mali imo katika hali mzozo wa kisiasa na kijamii. Hakuna nafasi tena ya kufanya makosa." Goita aliwaambia waandishi habari huku akiwa amezungukwa na wanajeshi. Umoja wa Afrika umeshutumu kile ilichosema kuwa ni "mabadiliko ya serikali ambayo ni kinyume na katiba" nchini Mali.
Kundi hilo la mataifa limetangaza kuwa linasimamisha uanachama wa Mali , ikiwa ni hatua ambayo si ya kawida inayomzuwia mwanachama kuhudhuria mikutano yote ya kilele na mikutano ya kawaida, "hadi pale utaratibu wa kikatiba utakaporejeshwa." Waziri wa mambo ya kigeni waq Niger Kalla Ankourao ameeleza kusikitishwa kwa jumuiya ya ECOWAS kutokana na mapinduzi hayo
Uongozi wa kijeshi wa Mali
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesisitiza wito wake jana wa kurejea katika utawala wa kiraia. Nae waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Heiko Maas amesema anaungana na Ufaransa na kundi la mataifa wanachama wa jumuiya ya ECOWAS kuwataka wanajeshi kurejesha uongozi wa kiraia.
"Tunazungumza na wenzetu wa Ufaransa ili kupata taarifa zaidi juu ya kutoa usaidizi kwa madai ya jumuiya ya ECOWAS kutaka kurejesha utawala wa kikatiba. Na kutokana na tathmini yetu ni lazima mapinduzi haya yasitishwe."
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alisema kuwa Marekani, inashutumu vikali uasi wa Agosti 8 nchini Mali kama tunavyoshutumu hatua yoyote ya kuchukua madarakani kwa nguvu."
Amesema uhuru na usalama wa maafisa wa serikali waliokamatwa pamoja na familia zao ni lazima uhakikishwe," amesema.
Mataifa 15 ya Jumuiya ya maendeleo ya Afrika magharibi ECOWAS , ambayo yamejaribu bila mafanikio kusimamia mapatano katika mzozo huo wa kisiasa wa muda mrefu , pia utasitisha uanachama wa mali katika vyombo vyake vya ndani vinavyofanya maamuzi.