1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamala Harris amshambulia Trump katika mkutano wa hadhara

24 Julai 2024

Mgombea wa urais wa chama cha Democratic, Kamala Harris amefanya mkutano wake wa kwanza wa kampeni tangu awe mgombea kwa kuanzisha mashambulizi mapya kwa Donald Trump kuwa anajiribu kuirejesha nyuma Marekani.

https://p.dw.com/p/4ieus
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris katika mkutano wa kampeni huko West Allis, Wisconsin
Makamu wa Rais Kamala Harris akitoa hotuba wakati wa hafla ya kampeni, katika Shule ya Sekondari ya West Allis Central, huko West Allis, Wisconsin, Marekani, Julai 23, 2024.Picha: Kevin Mohatt/REUTERS

Tofauti na mtangulizi wake rais anaeondoka madarakani, Joe Biden, ambae mara nyingi amekuwa akisitasita na kuzungumza kwa taratibu katika hotuba zake, Makamu wa Rais Kamala Harris alikuwa akihutubia kwa nguvu na hamasa, ambayo ilipokelewa kwa shangwe katika hafla hiyo katika uwanja  katika mkutano wake wa hadhara jimboni Wisconsin.

Kwa tathimini ya mkutano huu wa mwanzo wachambuzi wanahisi, Harris mwenye umri wa miaka 59, anaonesha mwenye kuongeza matumaini mapya katika chama cha Democratic, kufuatia Biden mwenye umri wa miaka 81 kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kushiriki mjadala mbaya na Trump uliozusha hofu kuhusu umri wake na uwezo wake wa kiakili.

Harris: Trump anataka kuirejesha Marekani nyuma

Kampeni ya uchaguzi ya Marekani l Kamala Harris katika mkutano wa kampeni huko West Allis, wafuasi wa Wisconsin
Wafuwasi wa Makamu wa Rais Kamala Harris, mteule wa chama cha Democratic, katika kampeni huko West Allis, WI, Julai 23, 2024.Picha: Dominic Gwinn/Middle East Images/picture alliance

Katika mkutano huo wa hadhara wa Milwaukee Kamala anasema Trump anataka kuirejesha Marekani nyuma, na kuwahoji wahudhuriaji kama wangependa kuishi katika nchi yenye uhuru, huruma na utawala wa sheria au nchi yenye machafuko, hofu na chuki? "Na sisi tunaoamini katika uhuru wa uzazi. Tutakomesha marufuku ya utoaji mimba ya Donald Trump, kwa sababu tunaamini katika wanawake kufanya maamuzi kuhusu miili yao na sio serikali yao kuwaambia la kufanya" Alisema Harris.

Wakati Biden alikuwa akimchukila Biden kama kitisho kikubwa cha demokrasia, Harris alichukua mkondo wa kibinafsi zaidi kwa kulenga ishara za rekodi yake kama mwendesha mashtaka wa California ambaye alishughulikia kile alichosema kuwa "wanyanyasaji" na "walaghai" kama rais wa zamani na mhalifu aliyewahi kuhukumiwa.

Kampeni za Republican zaonekana kuwa katika misukosuko

Kampeni za Trump zimeingia katika msukosuko baada ya Biden kujiweka kando, jambo ambalo sasa linamfanya kuwa mgombea mkongwe zaidi wa urais wa Marekani. Lakini mwenyewe Trump anasisitiza kwamba itakuwa rahisi zaidi kumshinda Harris katika uchaguzi wa Novemba kuliko  ilivyotarajiwa kwa Biden. Trump, ambaye alinusurika katika jaribio kuuwawa la Julai 13, pia aliwaambia waandishi wa habari kwamba pasi shaka atashiriki katika angalau mdahalo mmoja wa urais na Harris.

Wakati huohuo Rais Biden amerejea katika Ikulu ya Marekani White House baada ya kujitenga kwa takribani juma zima katika nyumba yake ya ufukweni ya Delaware, baada ya kupata maambukizi ya Covid, eneo ambalo alilitumia kutoa tangazo lake lililoshtusha la kujiondoa katika kinyang'anyiro cha urais.

Soma zaidi:Harris afanya kampeni katika jimbo la Wisconsin

Rais huyo wa sasa wa Marekani ametangaza pia kuwa Jumatano atatoa hotuba wa kwanza ambayo pamoja na mambo mengine ataweka wazi kwanini amejiengua katika kampeni za urais wa taifa lake, mahususi kwa uchaguzi wa Novemba.