1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Kamati ya Sudan yasema hadi watu 100 waliuawa kijijini

6 Juni 2024

Kamati ya wanaharakati wanaounga mkono demokrasia nchini Sudan imeripoti kwamba watu mia moja wameuwawa mnamo siku moja katika kijiji kilichoshambuliwa na wanajeshi.

https://p.dw.com/p/4gjyh
Mapigano Sudan
Umoja wa Mataifa unaonya kuhusu baa la njaa na watu kuyahama makaazi yao nchini Sudan.Picha: Albert Gonzalez Faran/Unamid/Han/dpa/picture alliance

Kamati ya wanaharakati ya Madani imesema wanamgambo wa RSF, walikishambulia mara mbili kijiji cha kati cha Wad al-Noura katika jimbo la al-Jazira kwa silaha nzito. Mashambulizi hayo yamesababisha maafa na watu kadhaa kuyahama makaazi yao.

Katika taarifa yake jana Jumatano, kundi la wanamgambo wa RSFlilisema lilishambulia kambi tatu za jeshi katika eneo la Wad al-Noura. Jeshi na wanamgambo wa RSF wameshutumiwa kwa uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kuwalenga raia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji lilionya leo Alhamisi kwamba idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Sudan inaweza kufikia milioni kumi ndani ya siku chache.