CERD yaelezea wasiwasi kuhusu soka ya Italia
1 Septemba 2023Katika taarifa, CERD imesema kuwa kuhusu Italia, imetiwa hofu na wanasiasa na maafisa wa ngazi za juu wa serikali wanaotumia matamshi ya chuki na mijadala ya kisiasa ya kibaguzi dhidi ya makabila madogo hasa Waroma, Wasinti na Camminanti, Waafrika na watu wa asili ya Kiafrika.
CERD yaelezea wasiwasi kuhusu ubaguzi katika michezo
Kamati hiyo pia imeelezea wasiwasi kuhusu visa vya ubaguzi wakati wa hafla za michezo vinavyojumuisha mashambulizi ya kimwili na maneno dhidi ya wanariadha wa asili ya Kiafrika.
CERD yataka waliohusika na ubaguzi kuwajibishwa
CERD, imeitaka Italia kuchunguza dhuluma zote za kibaguzi katika michezo na kuwawajibisha waliohusika.
Mwanachama mmoja wa kamati hiyo, Regine Esseneme, raia wa Cameroon, ameihimiza Italia kuzingatia kwa makini visa hivyo vya ubaguzi vinavyozidi kuongezeka dhidi ya watu weusi na watu wa asili ya Kiafrika.