1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA : Katiba yabadilishwa kumuwezesha Museveni kuwania tena Urais

13 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEv7

Bunge la Uganda hapo jana limefuta vikomo vya muhula wa Urais vilivyowekwa katika katiba ya nchi hiyo na hiyo kumsafishia njia Rais Yoweri Museveni katika harakati zake za kujaribu kuwania tena Urais hapo mwakani.

Hatua hiyo inakuja wakati Museveni akianzisha kampeni kwa wapiga kura kutenguwa kupigwa marufuku kwa demokrasia ya vyama vingi alikokuweka miaka 20 iliopita hatua ambayo wakosowaji wake wanadai kuwa ni jaribio la kuficha tamaa yake ya kugombania Urais na hatimae kuwa Rais wa maisha.

Msemaji wa bunge Bernard Aceru amesema wabunge wamepiga kura 220 kutowa idhini ya mwisho kwa marekebisho ya katiba ambayo yanafuta muda wa vipindi viwili vya Urais. Wabunge 43 walipinga na wawili hawakushiriki.