KAMPALA: Museveni afungua mkutano wa jukwaa la biashara la Commonwealth
20 Novemba 2007Matangazo
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amewambia wanachama wa jumuiya ya madola Commonwealth waondoe vikwazo vya kiuchumi vinavyozizuia nchi maskini kuuza bidhaa zao katika mataifa ya kigeni.
Rais Museveni alikuwa akizungumza wakati alipoufungua mkutano wa jukwaa la kiuchumi kabla kuanza rasmi kwa mkutano wa 53 wa jumuiya ya madola mjini Kampala, Uganda. Rais Paul Kagame wa Rwanda na naibu wa jumuiya ya Commonwelath, Don McKinnon, pia wamehudhuria mkutano huo.
Mkutano wa leo unaonekana kama fursa nzuri kwa wawekezaji kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Commonwealth kupanua ushirikiano wao wa kibiashara .