1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA : Museveni azungumza na waasi kwa mara ya kwanza

11 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkH

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekuwa na mazungunmzo ya moja kwa moja kwa njia ya simu na uongozi wa juu wa kundi la waasi la LRA tokea kuanza kwa mapambano yao ya miaka 20.

Kwa kile mwakilishi wa waasi alichokiita kuwa hatua muhimu katika kujenga kuaminiana Mueseveni alikuwa na mazungumzo ya dakika 20 na Naibu Kiongozi wa LRA Vincent Otti hapo jana ambapo alisikiliza malalamiko juu ya jeshi kuwazingira waasi licha ya kuwepo kwa mazungumzo ya amani.

Martin Ojul mwakilishi ambaye ni mkuu wa ujumbe unaowawaklisha waasi katika mzungumzo hayo huko kusini mwa Sudan ameliambia shirika la habari la Uingereza Reuters kwamba hii ni mara ya kwanza na inaonyesha jinsi LRA ilivyo makini na mazungumzo hayo.