1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni ya kura ya maoni ya katiba yamalizika Burundi

Amida ISSA14 Mei 2018

Kampeni ya kura ya maoni ya katiba nchini Burundi imemalizika. Kura hiyo itafanyika Mei 17. Chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD kimeeleza kuridhishwa kwake na namna kampeni zilivyoendeshwa

https://p.dw.com/p/2xhXn
Burundi, Wahlkampfveranstaltung der CNDD-FDD
Picha: DW/K. Tiassou

Chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD kimeeleza kuridhishwa kwake na namna kampeni za kura ya maoni juu ya mbadiliko ya katiba zilivyoendeshwa kwa amani, katika siku ya mwisho ya kampeni kuelekea kura hiyo itakayofanyika Mei 17, huku upande wa upinzani ukikosoa hatua ya wafuasi wa CNDD-FDD kuuvamia msafara wa kiongozi wake aliekuwa anahamasisha wapigakura kupinga mabadiliko hayo Agathon Rwasa katika mkoa wa Karuzi.

Muda mchache kabla ya kampeni za uchaguzi juu ya kura ya maoni kuhitimishwa chama Cndd fdd kimerindima jijini Bujumbura. Chini ya usimamizi wa Evariste ndayishimiye ambapo wafuasi wa chama hicho wamejumuika kuhamasisha kura ya ndiyo.

Matamshi yalisalia yale yale ya kuwa katiba mpya itairuhusu Burundi kuachana na sera za kikoloni. Evariste Ndayishimiye amekaribisha na kusema kampeni imefanyika na kumalizika salama na kwamba ni ishara tosha kuwa nchi iko salama.

Baadhi ya viongozi wa upinzani Burundi
Baadhi ya viongozi wa upinzani BurundiPicha: DW/A. Niragira

Nao wapinzani wao ambao ni chama cha Amizero ya Abarundi kinachoongozwa na Agathon Rwasa kilionekana kuwavutia pia watu wengi kinyume na ilivyo tarajiwa, kimeendesha kampeni yake ya kutetea kura ya hapana kikiwa mkoni Gitega mji wa pili muhimu Burundi.

Agathon Rwasa amekosoa kuona wafadhili wakitajwa kuwa ni wakoloni wakati ndio walosaidia kupatikana kwa mktaba wa Arusha na kurejea kwa watawala wa sasa kutoka maguguni hadi Bujumbura.

Hiyo jamii ya kimataifa inaowekwa kando leo sio ilosaidia hadi mkataba wa Arusha kupatikana, sio ilowasidia kuwanyanyua kutoka maguguni hadi jijini Bujumbura, kuwapangishia najumba na kuwapa kikosi chakuwalinda. Kwanini zama hizo hawakuwaita wakoloni na leo wawe wakoni?

Agathon Rwasa ambae msafara wake kutoka mkoani Karuzi ulivamiwa na watu wanao sadikiwa kuwa wafuasi wa chama cndd Fdd amewataka kutambuwa kuwa kila raia anahaki ya kutetea kura ya ndio ama ya hapana.

Kura ya maoni ya katiba kufanyika Mei 17
Kura ya maoni ya katiba kufanyika Mei 17Picha: Getty Images/AFP/C. De Souza

Hayo ni wakati mkuu wa tume ya uchaguzi Pierre Claver Ndayicariye amesema raia wengi hawakujitokea kuchukuwa kadi zao za kupigaia kura ambapo muda wa utoaji ulimaliza jana. Mkuu huyo wa Ceni amewataka kwenda kwenye ofisi za ceni kimkoa na kitarafa na kwamba kadi zitaendelea kutolewa. Pia wale ambao kadi hazikuchapishwa wanao haki ya kupiga kura mei 17.

Wakati uchaguzi huo ukisubiriwa watu 26 waliuwawa mishoni mwa wiki katika kijiji cha Ruhagarika mkoani Cibitoke baadda ya kushambuliwa na watu wenye silaha kutoka DRC. Miongoni mwa walo uwawa 12 ni kutoka familia moja ya afisa wa jeshi mlinzi wa rais Nkurunziza. Serikali imesema kushauriana na wakuu wa DRC ili waweze kukabiliana na waloendesha shambulio hilo.

Mwadishi: Amida ISSA - DW BUJUMBURA

Mhariri: Iddi Ssessanga