Kansela Gerhard Schröder akutana na waziri mkuu wa Uengereza Tony blair mjini Berlin
14 Juni 2005Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani na waziri mkuu Tony Blair wa Uengereza wamejaribu kupunguza makali ya mvutano kuhusu bajeti ya umoja wa Ulaya.Katika mkutanao wao mjini Berlin viongozi hao wawili wamezungumzia umuhimu wa kufikiwa maridhiano bila ya kupendelewa upande wowote.Hata hivyo waziri mkuu Tony Blair hakuonyesha ishara kama yuko tayari kuridhia madai ya nchi nyengine zanachama zinazopendelea ruzuku inazopokea Uengereza toka umoja wa ulaya zipunguzwe.Waziri mkuu wa Uengereza ametaka pia ruzuku za kilimo zinazoifaidisha zaidi Ufaransa,zipunguzwe.Hoja hizo zimepingwa na kansela Gerhard Schröder kwa kuzingatia maridhiano yaliyofikiwa mwaka 2002.Ufumbuzi wa mzozo wa bajeti ni mojawapo ya mitihani inayowakabili viongozi wa taifa na serikali watakapokutana mjini Brussels June 16 na 17 ijayo.