Kansela Scholz auonya upinzani dhidi ya suala la uhamiaji
30 Novemba 2024Matangazo
Suala la uhamiaji linatarajiwa kuchukua nafasi na ushawishi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu, mwaka ujao.
Scholz amesema kwenye mkutano wa kampeni hii leo kwamba upande wa upinzani wa vyama vya CDU/CSU unatishia kubadilisha sera ya sasa kwa sababu hautaki kukubaliana na uhalisia.
Amewaambia wawakilishi karibu 500 wa chama hicho katika makao makuu ya chama mjini Berlin kwamba Ujerumani kwa muda mrefu imekuwa ikiwategemea wahamiaji, akiwaangazia karibu wakazi milioni 25 wenye asili ya uhamiaji.
Ujerumani inataraji kufanya uchaguzi Februari 23 kufuatia kura ya imani ya bunge ya mwezi Disemba.