1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Scholz ahofia kutumwa wanajeshi wa Korea kaskazini, Ukraine

26 Oktoba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema ripoti za kupelekwa kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi "zinatia wasiwasi mkubwa."

https://p.dw.com/p/4mFkI
Rais Vladimir Putin azuru Korea Kaskazini
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na Rais wa Urusi Vladimir Putin wakikagua gwaride katika sherehe rasmi za kumkaribisha Putin katika ziara ya kiserikali nchini Korea KaskaziniPicha: Vladimir Smirnov/POOL/TASS/dpa/picture alliance

Kansela Scholz amewaambia waandishi wa habari akiwa ziarani nchini India kwamba ripoti hizo hazipaswi kupuuzwa, ingawa zinaashiria kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin yuko katika hali mbaya.

Kansela Scholz aidha amesema hatua hiyo pia ichukuliwe kama sababu ya kuongezwa jitihada za kupata amani, huku akiahidi kuendelea kuisaidia Ukraine.

Katika hatua nyingine, kumeripotiwa shambulizi la droni za Urusi kwenye jengo la makazi mjini Kyiv na kusababisha jengo hilo kuwaka moto.