Kansela Schröder ziarani mjini Prag
18 Mei 2005Matangazo
Kansela Gerhard Schröder na waziri mkuu wa jamhuri ya Tcheki Jiri PAROUBEK wameitembelea kambi ya zamani ya mateso ya Theresienstadt,kuwakumbuka wahanga wa utawala wa kinazi.Viongozi hao wawili wameweka shada la mauwa katika kiunga cha makaburi ya taifa umbali wa kilomita 60 toka mji mkuu wa jamhuri ya Tcheki-Prag.Mapema mwezi huu iliadhimishwa miaka 60 tangu kambi hiyo ya mateso ilipokombolewa.