Kansela Olaf Scholz leo atampokea Rais wa Argentina
23 Juni 2024Awali Milei alitarajiwa kupokewa kikamilifu kwa heshma za kijeshi, lakini hilo, pamoja na mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari, vilifutwa kwa taarifa fupi.
Badala yake duru zinaeleza kuwa, viongozi hao wawili wanatarajiwa kukutana kwa mazungumzo yaliyopangwa kudumu saa moja tu, ikielezwa kwa ombi la Milei.
Mkutano kati ya viongozi hao wawili wanaotofautiana sana kiitikadi utalenga katika masuala ya uwezekano ya kiuchumi. Argentina ina akiba kubwa ya malighafi ya madini kama lithiamu ambayo yanahitajika sanakwa Ujerumani katika kipindi hiki cha Ujerumani kujiondoa katika utegemezi wa nishati kutoka Urusi.
Rais Milei, ambae alichaguliwa kwa zaidi ya asilimia 55 ya kura katika uchaguzi wa Novemba aliwasili nchini Ujerumani jana Jumamosi kwa shabaha ya kupokea medali kutoka kwa Wakfu wa Friedrich August von Hayek huko kaskazini mji wa bandari wa Hamburg.