1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kasfha zisizokwisha za madini ya Congo

Kiswahili15 Februari 2022

Mwezi Septemba,Rais wa Kongo Félix Tshisekedi aliitaka serikali yake kuchukua hatua kukomesha uchimbaji haramu wa madini,Lakini agizo hilo halionekani kutekelezwa.

https://p.dw.com/p/473Vq
Kashfa kuhusu mzozo wa madini inahusisha hata familia na washauri wakaribu wa Tshisekedi
Kashfa kuhusu mzozo wa madini inahusisha hata familia na washauri wakaribu wa TshisekediPicha: Getty Images/AFP/P. Moore

Hata kama ni taarifa chache zilizo jitokeza wiki mbili baada ya kukamatwa na kuhojiwa kwa François Beya, mshauri maalum wa Rais Félix Tshisekedi, vyanzo kadhaa vinaibua ushindani mkali wa ushawishi ulioko baina ya washauri wa Rais.

Kulingana na gazeti la kila wiki la Jeune Afrique, mmoja ya washauri wa karibu wa Tshisekedi alisema kunamvutano wa usimamizi wa kandarasi za uchimbaji madini.

Toka mwezi Novemba, Francois Beya alikosolewa vikali na wasaidizi wengine wa rais baada ya uchunguzi alioendesha kuhusu mzozo wa madini kati ya washauri wa rais Tshisekedi.

Soma Pia→DRC yasema haitaruhusu madini yake kuchakatwa nje ya Afrika

''Kesi zinazohusiana na madini''

Mazingira magumu ya wachimbaji madini nchini Kongo
Mazingira magumu ya wachimbaji madini nchini KongoPicha: Getty Images/J. Kannah

Mills Tshibangu, mwandishi wa habari za uchunguzi katika Mkoa wa madini wa Haut-Katanga, anasema wanasiasa kadhaa, wakiwemo watu wa karibu na rais, wanajihusisha na uchimbaji madini.Tshibangu amesema, kujiuzulu mwezi uliopita kwa Jean-Marc Kabund,mwenyekiti wa chama tawala, kutoka wadhifa wake kama makamu wa Spika wa Bunge kunahusishwa haswa na mizozo ya masilahi ya madini.

''Ametuhumiwa kwa kashfa nyingi za uchimbaji madini kinyume cha sheria. Hakika, kuna pia katika kujiuzulu kwa Kabund kesi zinazohusiana na madini.'' alisema Tshibangu.

Akihutubia wafuasi wa chama cha upinzani cha Ecidé cha Martin Fayulu,katibu mkuu wa chama hicho Devos Kitoko, aliwataka wafuasi wao kutoamini mivutano inayoendelea hivi sasa kwenye ikulu ya Rais Tshisekedi. Kitoko amesema ni migogoro ya ndani kwa ajili ya udhibiti wa maeneo ya uchimbaji madini.

Soma pia→Kampuni sita za Kichina za madini zafungiwa Congo

Wanani wanaofaidika na madini ya Congo?

Kuongezeka kwa wachimbaji migodi haramu
Kuongezeka kwa wachimbaji migodi haramuPicha: Getty Images/AFP/F. Scoppa

Ikiwa siku za nyuma watu wa familia ya Rais wa zamani Joseph Kabila walishutumiwa kwa kunyakua makumi ya kandarasi za uchimbaji madini, wanaharakati wa mashirika ya kiraia sasa wanaamini kuwa hakuna kilichobadilika toka utawala mpya wa Tshisekedi. Jean-Claude Mputu,msemaji wa shirika  ''Le Congo n'est pas à Vendre'' (Kongo sio ya kuuza ),la kupambana na rushwa nchini Kongo,amesema agizo la Tshikesedi kwa serikali yake ili kusitisha uchimbaji haramu wa madani halijatekelezwa.

''Mashirika ya kiraia kwenye mikoa ya Lualaba, na huko Haut-Katanga, wanalaani ushawishi wa watu wa karibu na washirika wa Rais katika umilikaji migodi na uchimbaji madini kwa kushirikiana na Wachina au wafanyabiashara wengine. Kwa hivyo tuko kwenye mwendelezo,badala ya mabadiliko. Kilichobadilika ni kwamba tunamvua nguo Mtakatifu Paulo ili kumvika Mtakatifu Yoana.'' alisema Mputu.

Ripoti kadhaa zinadai kuwa wafanyabiashara, wanasiasa na maafisa wa kijeshi wanahusika na uchimbaji madini nchini Kongo.