1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

Katiba mpya ya Chad yaidhinishwa kwa asilimia 86 ya kura

25 Desemba 2023

Tume ya Uchaguzi nchini Chad imetangaza kwamba rasimu ya katiba mpya iliyopigiwa kura wiki moja iliyopita imeidhinishwa kwa asilimi 86 lakini matokeo hayo yamepingwa mara moja na viongozi kadhaa wa upinzani.

https://p.dw.com/p/4aY91
Bendera ya Chad.
Bendera ya Chad.Picha: Mohamed Messara/dpa/picture-alliance

Tangazo la tume hiyo limesema idadi ya wapigakura waliojitokeza ilikuwa asilimia 63.75 na kwamba licha ya "hitilafu ndogo" zilizoshuhudiwa, kura hiyo ya maoni ilifanyika vizuri. Matokeo rasmi ya kura hiyo yatasubiri kuidhinishwa na Mahakama ya Juu ya taifa hilo mnamo Disemba 28.

Watawala wa kijeshi wa Chad wameipigia upatu katiba iliyopitishwa kuwa hatua muhimu kuelekea kuirejesha Chad chini ya utawala wa kiraia. Hata hivyo upinzani na wanaharakati wengine wameyapinga madai hayo na walitoa mwito wa kususiwa kura ya maoni iliyofanyika Disemba 17.

Upinzani pia umeyapinga matokeo ya kura hiyo na umesema takwimu zilizotolewa juu ya idadi ya wapiga kura ni za uongo.