Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya, IEBC imewafuta kazi maafisa wake wanne ambao waligundulika kufanya mkutano wa faragha nyumbani kwa mgombea wa nafasi ya uwakilishi wa bunge la kaunti huko Homa Bay. Tume hiyo imesema maafisa hao wamekiuka sheria kwa sababu hawatakiwi kuegemea upande wa kisiasa. Sikiliza mahojiano kati ya Hawa Bihoga, na mwandishi James Omoro aliyeko Homa Bay.