Shughuli ya kuwahoji mawaziri wapya imeanza rasmi hii leo. Kila mmoja ana muda wa saa mbili kujieleza mbele ya kamati ya bunge ya uteuzi. Zoezi hilo litaendelea hadi Jumamosi ili mawaziri wateule wote 22 wapate fursa ya kujieleza. Bunge limepewa muda hadi mwanzoni mwa Novemba kutoa ridhaa yao kabla ya ripoti kamili kuwasilishwa kwa Rais Ruto. Sikiliza ripoti ya Thelma Mwadzaya kutoka Nairobi.