Kenya yaadhimisha miaka 60 ya kuwa Jamhuri
12 Desemba 2024Akiongoza sherehe hizo Rais William Ruto wa Kenya amesema, atawafikia Wakenya wote bila kujali mirengo yao ya kisiasa kwa lengo la kuwa na taifa dhabiti na imara.
Ruto aliongeza kuwa wanaoikosoa serikali yake wanastahili kusema ukweli badala ya kueneza habari za uwongo.
Hotuba yake Ruto inajiri siku chache baada ya
Rais Ruto na mtangulizi wake Uhuru hawajakuwa wakionana uso kwa macho tangu Ruto achukue mikoba ya uongozi mwaka 2022.
Aidha Rais Ruto alikutana na viongozi wa dini siku ya Alhamisi kwenye ikulu ya Nairobi ishara ya kutaka kupunguza joto ambalo vongozi hao wamekuwa wakimpulizia kwa kuendekeza mauaji ya kiholea, utekaji nyara, kupanda kwa gharama ya maisha pamoja na kuongezeka kwa ufisadi.
Kwenye sherehe za Jamhuri Rais wa Gambia, Adama Barrow, alikuwa mgeni mwalikwa mwaka huu. Wageni wengine mashuhuri ni pamoja na Huldah Momanyi, Mwakilishi wa Bunge la Minnesota, na wawakilishi wa kidiplomasia kutoka mataifa mbalimbali.
Ruto asifu mafanikio ya serikali yake baada ya miaka miwili madarakani
Kwenye hotuba iliyochukua takriban saa moja Rais Ruto alitumia muda huo kuelezea mafanikio ambayo serikali yake imefikia kwa kipindi cha miaka miwili.
"Nitaendelea kufikia Wakenya kutoka kila nyanja ya maisha, bila kujali mirengo yao ya kisiasa kwa lengo la kuwa na taifa dhabiti na kuhakikisha mbegu imara siku za baadaye.”
Wakenya wa matabaka mbali mbali wamekuwa wakizikosoa sera za serikali inayotawala ya Jubilee kwa gharama kubwa ya maisha na kuongeza kodi.
Hata hivyo Rais Ruto aliwakosoa kwa kudai kuwa wanatumia maelezo ya uwongo kueneza habari potovu. Alisema kuwa kwamba gharama ya bidhaa za msingi za chakula imeshuka akiongeza kuwa mfumuko wa bei umepungua.
"Siku ya Jamhuri ni wakati wa Wakenya kuangazia habari ghushi, zinazolenga kusambaratisha ufanisi wetu, kuhujumu matumaini yetu na kupunguza ari yetu.”
Wakenya kutoka sehemu mbalimbali za nchi wamehudhuria sherehe za leo.