Kenya yaangamiza bunduki 5,000
16 Novemba 2016Matangazo
Ruto aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba serikali imeteketeza bunduki hizo hadharani ili kutuma ujumbe kwa wale wanaofanya biashara haramu ya silaha.
Makamu huyo wa rais amesema silaha ndogo ndogo zinaleta kitisho kwa amani na utulivu wa Kenya kwa sababu zimekuwa ni rahisi kupatikana kwa bei nafuu na ni nyepesi kuzificha.
Silaha hizo zilizokamatwa kutoka kwa wahalifu au kusalimishwa kwa hiari ziliharibiwa mjini Ngong, kusini magharibi mwa mji mkuu, Nairobi.
Ruto amewataka wale wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha kwa jeshi la polisi.