1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yafungua mpaka na Ethiopia tena kuruhusu biashara

Daniel Gakuba
22 Januari 2021

Biashara zimeanza tena kwenye mji wa Moyale ambao uko katika mpaka kati ya Kenya na Ethiopia, baada ya serikali kuufungua mpaka huo.

https://p.dw.com/p/3oHKF
Wegweiser Autobahnschild Äthiopien
Picha: DW

Kulingana na naibu kamishna wa eneo la uwakilishi la Dukana, Solomon Mwapapale, mpaka huo ulifunguliwa baada ya mazungumzo kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.

Mwapapale amesema serikali inanuia kuhakikisha kuna usalama wa kutosha na uhuru wa watu kusafiri kati ya mataifa hayo mawili. Hata hivyo, afisa huyo amesema serikali haitaruhusu biashara haramu kuendeshwa kwenye eneo hilo la mpakani.

Ikumbukwe kuwa mpaka wa Kenya na Ethiopia umekuwa ukitumika na wanaofanya biashara ya binadamu pamoja na walanguzi wa dawa za kulevya

Mpaka huo ulifungwa kutokana na changamoto za kiusalama hasa nchini Ethiopia, pamoja na hofu ya kusambaa kwa virusi vya corona.